Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati amepata kibali cha ajira kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kupitia barua yenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/A/25 ya tarehe 29/04/2025 kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Anaalika Watanzania wenye sifa kuomba nafasi zifuatazo:
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
1. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II – Nafasi 3
Majukumu ya Kazi:
- Kuchapa barua na nyaraka za kawaida na siri
- Kupokea wageni na kuelekeza wanapopaswa kwenda
- Kutunza kumbukumbu, ratiba na miadi ya mkuu wake
- Kusimamia majalada na nyaraka za idara
- Kuandaa dondoo, vifaa na maandalizi ya vikao
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha IV au VI
- Stashahada (Diploma) ya Uhazili au NTA Level 6 ya Uhazili
- Uwezo wa kuchapa maneno 100 kwa dakika kwa Kiswahili na Kiingereza
- Maarifa ya programu za ofisi (Word, Excel, PowerPoint, Email, Publisher n.k.)
- Mafunzo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali
Mshahara: TGS C
2. Dereva Daraja II – Nafasi 4
Majukumu ya Kazi:
- Kukagua usalama wa gari kabla na baada ya safari
- Kuwasafirisha watumishi kikazi
- Kufanya matengenezo madogo ya gari
- Kutunza log book ya safari
- Kusambaza nyaraka na kufanya usafi wa gari
- Majukumu mengine kutoka kwa msimamizi
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha IV
- Leseni ya Daraja E au C
- Uzoefu wa mwaka 1 bila kusababisha ajali
- Cheti cha Basic Driving Course kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa
Mshahara: TGS B
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Raia wa Tanzania, umri miaka 18 hadi 45
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja aina ya ulemavu
- Ambatanisha CV yenye namba za simu, email, na referees watatu
- Ambatanisha vyeti halisi vilivyothibitishwa na wakili:
- Cheti cha Kidato cha Nne/Sita
- Vyeti vya taaluma na kompyuta
- Cheti cha mafunzo ya udereva (kwa nafasi ya Dereva)
- Testimonials, Provisional Results, Statement of Results hazitakubaliwa
- Waliosoma nje wahakikishe vyeti vimeidhinishwa na NECTA, TCU au NACTVET
- Wastaafu hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
- Watumishi wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba
- Taarifa au vyeti vya kughushi vitasababisha hatua za kisheria
- Tafauti za majina kwenye vyeti zirekebishwe kwa Deed Poll
Jinsi ya kutuma maombi
Mwisho wa Kutuma Maombi
Tarehe ya mwisho: 14/08/2025
Namna ya Kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kwa njia ya mfumo wa kielektroniki kupitia:
https://portal.ajira.go.tz
Anuani ya barua ya maombi:
Mkurugenzi wa Mji
S.L.P 383
BABATI
Maombi yasiyotumwa kwa mfumo huu hayatafanyiwa kazi.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments