Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mji Rufiji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Rufiji anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi kwa kada mbili (02) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
Kada | Idadi ya Nafasi | Sifa za Mwombaji | Ngazi ya Mshahara |
---|---|---|---|
Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II(Office Management Secretary II) | 06 | – Kidato cha IV au VI- Diploma/Uhazili NTA Level 6- Ujuzi wa Hatimkato (Kiswahili & Kiingereza – maneno 100/dakika)- Mafunzo ya Kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher) kutoka chuo kinachotambulika na Serikali | TGS C |
Dereva Daraja II(Driver II) | 04 | – Kidato cha IV- Leseni Daraja E au C- Uzoefu wa angalau mwaka 1 bila ajali- Vyeti vya Mafunzo ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambulika na Serikali | TGS B |
Masharti ya Jumla
- Awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18–45.
- Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na waainishe ulemavu wao.
- Wasilisha C.V yenye mawasiliano sahihi na wadhamini watatu wa kuaminika.
- Vyeti vya elimu na taaluma vihalalishwe na Mwanasheria/Wakili.
- Vyeti vya nje vihalalishwe na TCU, NECTA au NACTVET.
- Wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Jinsi ya kutuma maombi
Maombi yatatumwa kupitia mfumo wa kielektroniki: https://portal.ajira.go.tz.
Mwisho wa kutuma maombi: 08 Oktoba, 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments