Nafasi za Kazi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NOAT)

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NOAT), Sekretarieti ya Ajira inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki kujaza nafasi 73 kama ifuatavyo:

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

1. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Hesabu) – Nafasi 55

  • Shahada ya Uhasibu / Stashahada ya Juu ya Uhasibu au Shahada ya Sayansi ya Menejimenti ya Kodi

2. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Usalama wa Mifumo ya TEHAMA) – Nafasi 5

  • Shahada/Stashahada ya Juu ya Usalama wa Mtandao/Usalama wa TEHAMA, CEH, CCNA Security

3. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Kiuchunguzi – Utengenezaji Programu) – Nafasi 1

  • Shahada/Stashahada ya Juu ya TEHAMA – Software Development, ujuzi wa Java EE, C#, C++, Python, RDMS

4. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Usanifu wa Majengo) – Nafasi 1

  • Shahada/Stashahada ya Juu ya Usanifu wa Majengo, usajili wa bodi husika

5. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Uhandisi wa Mitambo) – Nafasi 1

  • Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi Mitambo

6. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Uchumi) – Nafasi 3

  • Shahada/Stashahada ya Juu ya Uchumi, Takwimu, Uchumi Kilimo

7. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Uhandisi wa Ujenzi) – Nafasi 3

  • Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi wa Ujenzi

8. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Uhandisi wa Migodi) – Nafasi 1

  • Shahada/Stashahada ya Uhandisi wa Migodi

9. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Mipango Miji) – Nafasi 1

Shahada/Stashahada ya Juu ya Upangaji Miji na Maeneo ya Ardhi

10. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Uhandisi wa Umeme) – Nafasi 1

  • Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi wa Umeme

11. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Uhandisi wa Mawasiliano) – Nafasi 1

  • Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi wa Mawasiliano

Masharti ya Jumla

  • Raia wa Tanzania, umri ≤ miaka 45 (isipokuwa watumishi wa umma).
  • Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba.
  • Waambatishe barua ya maombi, CV, vyeti halisi vilivyothibitishwa (kuzaliwa, elimu, taaluma).
  • Vyeti vya nje vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE.
  • Hakuna kupokea result slips au testimonials.

Jinsi ya Kutuma maombi

Mwisho wa kutuma maombi: 21 Agosti 2025

Maombi yatumwe kupitia Recruitment Portal: http://portal.ajira.go.tz

Soma zaidi: