Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi ya Dereva Daraja la II baada ya kupokea kibali cha ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
1. Dereva Daraja la II – Nafasi 3
Kazi na Majukumu:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari.
- Kuwasafirisha watumishi kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo ya gari.
- Kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kutunza taarifa za safari.
- Kusafisha gari.
- Kazi nyingine zitakazoelekezwa na msimamizi.
Sifa za Mwombaji
- Awe na elimu ya kidato cha nne (Form IV).
- Leseni ya daraja la ‘E’ au ‘C’.
- Uzoefu wa kuendesha angalau kwa mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
- Cheti cha mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Ngazi ya Mshahara: TGS B
Masharti ya Jumla
- Awe Mtanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja aina ya ulemavu.
- Ambatishe wasifu binafsi (CV), namba za simu na wadhamini (referees).
- Waliopo kazini Serikalini hawaruhusiwi kuomba.
- Ambatishe vyeti halisi vilivyothibitishwa na wakili (Form IV, V, taaluma).
- Vyeti kama Testimonials na Statement of Results havitakubaliwa.
- Waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU/NECTA/NACTE.
- Wastaafu hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Wanaotumia majina tofauti waambatishe Deed Poll au Affidavit.
- Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
Jinsi ya kutuma maombi
Mwisho wa Kutuma Maombi
Tarehe ya mwisho: 14/08/2025
Namna ya Kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kwa njia ya mfumo wa kielektroniki kupitia:
https://portal.ajira.go.tz
Anuani ya barua ya maombi:
Mkurugenzi wa Manispaa,
Manispaa ya Kigoma Ujiji,
S.L.P 44,
KIGOMA.
Maombi yasiyotumwa kwa mfumo huu hayatafanyiwa kazi.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments