Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanzishwa chini ya Kifungu cha 2(1) cha National Identification Authority (Establishment) Instrument, 2008. Inafanya kazi chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (MoHA) ikiwa na jukumu la kusajili, kutambua na kutoa Vitambulisho vya Taifa kwa raia wa Tanzania, wakazi wa kudumu na wakimbizi wanaostahiki. Pia, NIDA inahifadhi na kusimamia hifadhidata ya Taifa ili kuimarisha amani, usalama na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
Nafasi | Idadi | Mwajiri | Tarehe ya Mwisho Kutuma Maombi |
---|---|---|---|
Afisa TEHAMA Daraja la II – Mendelezaji Mifumo (Systems Developer) | 3 | NIDA | 22 Agosti 2025 |
Afisa TEHAMA Daraja la II – Msimamizi wa Hifadhidata (Database Administrator) | 1 | NIDA | 22 Agosti 2025 |
Afisa TEHAMA Daraja la II – Msimamizi wa Mifumo (Systems Administrator) | 4 | NIDA | 22 Agosti 2025 |
Masharti ya Jumla ya Maombi:
- Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja hali yao wazi kwenye mfumo wa maombi.
- Ambatanisha CV yenye taarifa sahihi za mawasiliano, anwani, barua pepe na simu.
- Maombi yaambatanishwe na nakala zilizohakikiwa za vyeti vya kitaaluma (Postgraduate, Shahada, Diploma, Cheti), matokeo ya kitaaluma, vyeti vya kidato cha IV na VI, vyeti vya usajili (kama inahitajika), na cheti cha kuzaliwa.
- Haikubaliki kuambatanisha results slips, testimonials au partial transcripts.
- Weka pasipoti-size picha ya hivi karibuni kwenye mfumo wa maombi.
- Watumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
- Wastaafu wa utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
- Taja waamuzi watatu (referees) wenye mawasiliano sahihi.
- Vyeti vya shule vilivyotolewa nje ya nchi vihakikiwe na NECTA; vyeti vya kitaaluma vihakikiwe na TCU au NACTE.
- Barua ya maombi iwe na sahihi, iandikwe Kiswahili au Kiingereza
- Walioteuliwa tu ndio watajulishwa tarehe ya usaili.
- Nyaraka au taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
Jinsi ya kutuma maombi
Maombi yote yatumiwe kupitia Recruitment Portal: http://portal.ajira.go.tz/ (pia inapatikana kupitia tovuti ya PSRS kwa kubofya Recruitment Portal).
Mwisho wa kupokea maombi: 22 Agosti 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments