Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Jeshi la Magereza Tanzania limefungua rasmi nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) pamoja na wahitimu wa Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree) katika fani mbalimbali.
Tangazo hili limetolewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza tarehe 15 Agosti 2025, na mwisho wa kutuma maombi ni 29 Agosti 2025.
Jeshi la Magereza
Kuhusu, Jeshi la Magereza lilianzishwa rasmi mwezi Agosti 25,1931 baada ya mgawanyo wa majeshi ya Polisi na Magereza kutokea. Licha ya kuwa na majukumu ya kulinda usalama na mali za wageni, kabla ya mwaka 1931 Jeshi la Polisi lilifanya pia kazi za Magereza kama zilivyokuwa kwa tafsiri na madhumuni ya wakoloni. Jeshi la Magereza wakati lilipoanzishwa liliitwa Idara ya Jela ambapo shughuli zake zilibaki kuwa zile za kikoloni za utesaji wa wafungwa pamoja na kazi ngumu bila kujali kama ni ya manufaa kwao au kwa Taifa.
Sifa za Waombaji
- Awe raia wa Tanzania mwenye Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
- Asiwe amewahi kuajiriwa Serikalini.
- Umri kati ya 18–24 (kwa Kidato cha Nne) na 18–28 (kwa wenye ujuzi maalum).
- Awe na Cheti cha Kuzaliwa na afya njema ya mwili na akili.
- Kiwango cha urefu: wanaume futi 5’7”, wanawake futi 5’4”.
- Asiwe ameoa/kuolewa au kuwa na watoto.
- Asiwe na tattoo/alama mwilini na asiwe na rekodi ya jinai.
- Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya uaskari magereza na kufanya kazi sehemu yoyote Tanzania Bara.
Fani na Ujuzi Unaohitajika
Jedwali lifuatalo linaonyesha fani zinazotakiwa kwa ngazi tofauti:
Ngazi ya Elimu | Fani Zinazohitajika |
---|---|
Shahada (Degree) | Software Engineering, Multimedia Technology & Animation, Cyber Security, Network Engineering, Psychology & Counselling, Mining Engineering |
Stashahada (Diploma) | Office Machine, Sign Language, Nursing, Agro-mechanization, Agriculture, Animal Health & Production |
Astashahada (Cheti) | Secretarial Studies (Katibu Muhtasi) |
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wote wanapaswa kuwasilisha maombi kupitia Mfumo wa Ajira wa Magereza (TPSRMS) kupitia kiunganishi:
Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatapokelewa.
Maelekezo Muhimu
- Waombaji waliowahi kufukuzwa mafunzo ya awali ya uaskari hawaruhusiwi kuomba tena.
- Mtu yeyote atakayewasilisha nyaraka za kughushi au taarifa za uongo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mwisho wa Kutuma Maombi
29 Agosti 2025
Tangazo hili limetolewa na:
Jeremiah Y. Katungu, ndc
Kamishna Jenerali wa Magereza
15 Agosti 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments