Nafasi za Kazi Chuo Kikuu SUA

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilianzishwa tarehe 1 Julai 1984 kwa Sheria ya Bunge Na. 6 ya mwaka huo, ambayo ilifutwa na Sheria ya Vyuo Vikuu Na.7 ya mwaka 2005. Kupitia sheria hiyo, SUA ilipata Katiba yake mwaka 2007.

Dira ya SUA ni kuwa Chuo Kikuu kinachoongoza katika utoaji wa elimu bora, ujuzi na ubunifu katika kilimo na sayansi shirikishi.

SUA inakaribisha maombi ya ajira kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki ili kujaza nafasi mbalimbali za kitaaluma zilizo wazi.

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

S/NNafasi ya KaziIdadi ya Nafasi
1Tutorial Assistant (Records and Archives Management)1
2Tutorial Assistant (Geomorphology)1
3Tutorial Assistant (Hydrogeology)1
4Tutorial Assistant (Bee Sciences)2
5Tutorial Assistant (Agriculture General)1
6Tutorial Assistant (Dairy Sciences)2
7Assistant Lecturer (Nutritional Epidemiology)2
8Tutorial Assistant (Plant Physiology)1
9Assistant Lecturer (Textile Design and Technology)1
10Assistant Lecturer (Agricultural Extension)1
11Tutorial Assistant (Plant Pathology)1
12Assistant Lecturer (Political Sciences)1
13Assistant Lecturer (Literature)1
14Tutorial Assistant (Agronomy)2
15Tutorial Assistant (Medicine)1
16Tutorial Assistant (Chemical and Process Engineering)1
17Assistant Lecturer (Educational Psychology and Counselling)2
18Assistant Lecturer (Curriculum and Instruction)1
19Tutorial Assistant (Civil and Water Resources Engineering)1
20Assistant Lecturer (Educational Foundations and Management)1
21Assistant Research Fellow (Agriculture/Natural Resources Management)1
22Assistant Lecturer (Wildlife Management)1
23Assistant Lecturer (Botany)1
24Lecturer – PhD (Agricultural Economics)1
25Assistant Lecturer (Agricultural Economics)2
26Assistant Lecturer (Mathematics)1
27Assistant Lecturer (Marketing)1
28Assistant Lecturer (Information Technology)1
29Assistant Lecturer (Trade)1
30Tutorial Assistant (Human Resource Management)1
31Tutorial Assistant (Statistics)1

Masharti ya Jumla ya Maombi:

  1. Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
  2. Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja hali yao wazi kwenye mfumo wa maombi.
  3. Ambatanisha CV yenye taarifa sahihi za mawasiliano, anwani, barua pepe na simu.
  4. Maombi yaambatanishwe na nakala zilizohakikiwa za vyeti vya kitaaluma (Postgraduate, Shahada, Diploma, Cheti), matokeo ya kitaaluma, vyeti vya kidato cha IV na VI, vyeti vya usajili (kama inahitajika), na cheti cha kuzaliwa.
  5. Haikubaliki kuambatanisha results slips, testimonials au partial transcripts.
  6. Weka pasipoti-size picha ya hivi karibuni kwenye mfumo wa maombi.
  7. Watumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
  8. Wastaafu wa utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
  9. Taja waamuzi watatu (referees) wenye mawasiliano sahihi.
  10. Vyeti vya shule vilivyotolewa nje ya nchi vihakikiwe na NECTA; vyeti vya kitaaluma vihakikiwe na TCU au NACTE.
  11. Barua ya maombi iwe na sahihi, iandikwe Kiswahili au Kiingereza
  12. Walioteuliwa tu ndio watajulishwa tarehe ya usaili.
  13. Nyaraka au taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yatumiwe kupitia Recruitment Portalhttp://portal.ajira.go.tz/ (pia inapatikana kupitia tovuti ya PSRS kwa kubofya Recruitment Portal).

Mwisho wa kupokea maombi: 02 Septemba 2025.

Soma zaidi: