Nafasi za kazi Kampuni ya Unitrans Tanzania Ltd ya jijini Dar es Salaam inatangaza nafasi za ajira kwa vijana 70 wa kiume na wa kike kama Madereva.
Nafasi: Madereva wa Malori (Truck Drivers) – 70 nafasi
Eneo la kazi: Kilombero
Aina ya Mkataba: Msimu (Seasonal)
Soma: Jinsi ya kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025 PSLE 2025/26
Majukumu:
- Kusafirisha miwa kutoka mashambani hadi kiwandani.
- Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na udereva zitakazopangwa.
Sifa za Mwombaji
- Awe na uelewa wa sheria na kanuni za usalama barabarani.
- Awe na leseni halali ya daraja E.
- Awe na uwezo wa kusoma na kuandika.
- Awe na cheti cha udereva wa magari makubwa (Rigid/HGV) kutoka chuo kinachotambulika na serikali.
- Awe na uzoefu wa angalau miaka 2 katika kuendesha malori.
- Umri kati ya miaka 25 – 45.
- Uwezo na utayari wa kufanya kazi usiku.
- Awe na barua ya uthibitisho wa leseni kutoka Jeshi la Polisi Tanzania.
Jinsi ya Kuomba
Wakilishi wanatakiwa kuwasilisha:
- Barua ya maombi
- Wasifu binafsi (CV)
- Nakala za vyeti husika
- Nakala ya cheti cha TIN
- Nakala ya kitambulisho cha NIDA
Anuani ya kutuma maombi:
Human Resources Manager
Unitrans Tanzania Ltd
P.O. Box 50, Kidatu
Au kwa barua pepe: iness.nangali@unitrans.co.tz
Mwisho wa kutuma maombi: 30 Septemba 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments