Nafasi za Jeshi JWTZ 2025

Nafasi za Jeshi JWTZ 2025
Nafasi za Jeshi JWTZ 2025

Nafasi za Kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za ajira kujiunga na jeshi kwa mwaka 2025 kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa stahiki. Tangazo hili linahusu vijana waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria au kwa mkataba wa kujitolea, pamoja na wale waliopo katika makambi ya JKT chini ya “Operesheni Jenerali Venance Mabeyo”.

Sifa za Waombaji

  • Raia wa Tanzania mwenye cheti halisi cha kuzaliwa.
  • Umri usiozidi miaka 25.
  • Afya nzuri na akili timamu.
  • Tabia na nidhamu nzuri, asiwe na rekodi ya makosa ya jinai.
  • Asiwe ameoa au kuolewa.
  • Asiwe amewahi kutumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM).
  • Awe amehitimu mafunzo ya JKT kwa mkataba wa miaka miwili au kwa mujibu wa sheria na kutunukiwa cheti.

Utaratibu wa Maombi

Kwa vijana waliopo makambini, utaratibu wa uandikishaji unaratibiwa na Makao Makuu ya Jeshi. Kwa waliomaliza mafunzo na kurejea nyumbani, wanashauriwa kufuatilia matangazo rasmi kupitia tovuti ya JWTZ: www.tpdf.mil.tz

Maelezo ya Ziada

Kwa maelezo zaidi, unaweza kuwasiliana na JWTZ kupitia:​

  • Simu: +255 737 962 064
  • Barua pepe: ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
  • Anuani: P.O. Box 194, Dodoma, Tanzania
  • Kwa taarifa kamili na ya hivi punde, tembelea tovuti rasmi ya JWTZ.

Soma zaidi: