Mpango wa Ufadhili wa Kujiendelea Watumishi Kada za Afya 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Mpango wa Ufadhili wa Kujiendelea Watumishi Kada za Afya 2025 Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaendelea kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Afya kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za matibabu, hususan ya kibingwa na ubingwa bobezi ndani ya nchi.

Kupitia mpango wa Samia Health Super-Specialization Program, Wizara ya Afya imejiwekea lengo la kusomesha wataalamu bingwa na bobezi wasiopungua 300 kila mwaka wa fedha. Hatua hii inalenga:

  • Kuimarisha na kusogeza huduma za afya kwa wananchi.
  • Kupunguza rufaa za matibabu nje ya nchi na gharama zake.
  • Kukuza fursa za tiba utalii nchini.

Kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Wizara imetengewa Shilingi Bilioni 9 kugharamia mafunzo ya wataalamu bingwa na bobezi (wanaoendelea na wapya).

Faida za Ufadhili

  1. Vyuo vya Ndani: Ada ya masomo na posho ya utafiti.
  2. Vyuo vya Nje ya Nchi: Ada ya masomo, nauli, posho ya kujikimu, na posho ya utafiti.

NB: Ufadhili huu sio mkopo, bali ni grant yenye masharti maalum ya kuendelea kutoa huduma nchini baada ya masomo.

Aina za Mafunzo Yanafadhiliwa

  • Ufadhili wa mtu mmoja mmoja kwa masomo ya ubingwa/kibobezi.
  • Ufadhili wa seti (kundi la wataalamu kutoka kada tofauti, wanaosomeshwa kwa pamoja ili kuanzisha huduma ya kibingwa/kibobezi katika hospitali).

Mfano: Huduma ya renal dialysis (kusafisha figo) ikihitaji madaktari bingwa wa figo, wauguzi, famasia, wataalamu wa maabara, ushauri nasaha, fiziotherapia na tiba kazi.

Vigezo vya Jumla vya Mwombaji

  1. Kuwasilisha maombi kupitia mfumo wa kielektroniki: https://esponsorship.moh.go.tz/
  2. Awe Raia wa Tanzania na Mtumishi wa Serikali.
  3. Awe na barua ya udahili (admission letter) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali (ndani au nje ya nchi).
  4. Awe anakwenda kusoma katika fani za kipaumbele zilizoainishwa na Wizara.
  5. Ufadhili utazingatia uhitaji na upungufu wa taaluma katika kituo cha kazi cha mwombaji.

Pakua PDF ya tangazo hapa.

Ratiba ya Maombi

  • Kuanza: 20 Agosti, 2025
  • Kufungwa: 12 Septemba, 2025
  • Njia ya maombi: Mfumo wa kielektroniki pekee

Shukrani

Wizara ya Afya, kwa niaba ya Sekta ya Afya nchini, inamshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kuliwezesha sekta ya afya katika maeneo ya miundombinu, rasilimali watu, dawa, vifaa tiba na vitendanishi. Wizara inaahidi kuhakikisha ndoto ya Mheshimiwa Rais ya kila mwananchi kupata huduma bora za afya na kwa ukaribu inatimia.

Soma zaidi: