Mfumo wa Maombi ya Ajira Polisi Tanzania 2025-26 Katika kuhakikisha uwazi na usawa kwa kila Mtanzania anayetaka kujiunga na Jeshi, serikali ya Tanzania imeanzisha mfumo rasmi wa maombi ya ajira unaopatikana mtandaoni. Mfumo huu ni sehemu ya jitihada za kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia, pamoja na kurahisisha upatikanaji wa fursa kwa vijana wa Kitanzania popote walipo.
Vigezo vya Kujiunga
Kwa mtu anayetamani kuwa askari wa Jeshi la Polisi, ni lazima awe na sifa zinazokubalika kisheria na kitaaluma. Miongoni mwa vigezo hivyo ni:
- Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
- Awe amehitimu kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2019 hadi 2024.
- Umri uwe kati ya miaka 18 hadi 25 kwa waliohitimu sekondari, na hadi miaka 30 kwa wenye elimu ya juu kama stashahada au shahada.
- Awe na afya njema ya mwili na akili, pamoja na urefu unaolingana: angalau futi 5’8” kwa wanaume na 5’4” kwa wanawake.
- Awe hajawahi kutiwa hatiani mahakamani wala kuwa na alama za kuchora mwilini (tattoo).
- Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya kijeshi na kufanya kazi kokote atakapopangiwa ndani ya nchi.
Maeneo Maalum ya Uhitaji
Jeshi la Polisi pia huwa na mahitaji maalum kwa fani mbalimbali, hasa kwa walio na elimu ya juu. Baadhi ya fani hizo ni pamoja na:
- Uhandisi wa Umeme, Mitambo na Mawasiliano
- Tiba na Sayansi za Afya (madaktari, wauguzi, wataalamu wa maabara)
- ICT na Usalama wa Mtandao
- Sheria na Uchunguzi wa Jinai
- Uandishi wa Habari na Lugha za kigeni kama Kifaransa, Kichina na Kireno
Jinsi ya Kutuma Maombi
Mchakato wa maombi hufanyika kwa njia ya mtandao kupitia tovuti maalum: https://ajira.tpf.go.tz. Mwandishi wa maombi anatakiwa kuandika barua kwa mkono (handwriting), kuiscan na kuiambatisha katika mfumo huo kwa njia ya PDF. Hatua hii inalenga kuthibitisha uhalisia wa muombaji.
Ni muhimu kutambua kwamba maombi yanayowasilishwa kwa njia ya barua pepe, posta au kwa mkono hayatakubaliwa. Aidha, mwombaji anatakiwa kufuatilia matangazo rasmi kutoka kwa Jeshi la Polisi kupitia tovuti yao au mitandao ya kijamii.
Mfumo huu wa maombi ya ajira si tu unarahisisha kazi bali pia unatoa nafasi kwa kila kijana mwenye ndoto ya kulitumikia taifa katika Jeshi la Polisi. Kwa kufuata taratibu stahiki na kujitayarisha mapema, kila mmoja ana nafasi ya kufanikisha ndoto yake ya kuwa sehemu ya chombo hiki muhimu cha usalama wa taifa.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments