Mfumo wa Maombi ya Ajira Magereza (TPS Recruitment Portal)

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Huu hapa Mfumo wa Maombi ya Ajira Magereza (TPS Recruitment Portal) Mwongozo huu umetayarishwa ili kutoa maelekezo wazi na rahisi kwa waombaji wanaotumia Tanzania Prisons Service Recruitment Management System (TPSRMS).

Unalenga kusaidia watumiaji kuingia, kusajili, na kutumia mfumo huu hatua kwa hatua ili kuhakikisha kila mmoja anaweza kuutumia ipasavyo.

Kila sehemu imeelezewa kwa undani na kufuatiwa na mfano au picha ili kurahisisha uelewa na matumizi bora ya mfumo.

Kuhusu Mfumo wa Ajira Magereza

Mfumo wa ajira magereza Tanzania Prisons Service Recruitment Management System (TPSRMS) ni mfumo wa mtandaoni ulioundwa ili kurahisisha na kidigitalisha mchakato wa ajira wa Jeshi la Magereza Tanzania.

Unaweza kufikiwa kupitia vifaa vyote vyenye intaneti kama vile:

  • Kompyuta (desktop/laptop),
  • Simu janja (smartphone),
  • Tablet.

Mfumo unamwezesha mwombaji wa kazi:

  • Kujisajili na kuthibitisha utambulisho wake kwa kutumia hifadhidata za taifa.
  • Kuwasilisha vyeti vya kielimu na kitaaluma.
  • Kuomba nafasi za kazi zinazotangazwa.
  • Kufuatilia hali ya maombi yake na kupata mrejesho.

TPSRMS umetengenezwa kwa kuzingatia uwazi, usalama na ufanisi ili kila mwenye sifa awe na nafasi sawa ya kuomba na kuzingatiwa kwenye ajira.

Kwa ufupi, manual hii inaelezea hatua kwa hatua jinsi waombaji wanaweza kutumia mfumo huu wa ajira za Magereza kuanzia usajili hadi kuangalia matokeo ya maombi yao. Yanafafanuliwa mambo yafuatayo:

Usajili (Registration)

  • Uthibitisho kwa kutumia NIDA na namba ya Mtihani wa Kidato cha Nne (NECTA).
  • Kujaza taarifa binafsi (namba ya simu, ndoa, makazi, email, n.k).
  • Kuunda akaunti na kuthibitisha kupitia email.

Uthibitisho wa Akaunti (Email Verification)

  • Kupokea link ya uthibitisho kutoka AJIRA MAGEREZA.
  • Kubofya link na kufikia Dashboard.

Kubadilisha Email au Kuboresha Taarifa

  • Ikiwa email iliyotumika si sahihi.
  • Kubadilisha nenosiri lililosahaulika (Forgot Password).

Kuingia (Login) na Dashboard

  • Kuona wasifu (profile), sifa za kitaaluma na hali ya maombi.

Kuongeza Sifa za Kielimu (Academic Qualifications)

  • Kidato cha Nne (Form IV) – huongezwa kiotomatiki.
  • Kidato cha Sita (Form VI) – kwa kuingiza Index Number na mwaka.
  • Cheti, Diploma na Shahada – kupitia NACTVET (kwa Cheti/Diploma) na TCU (kwa Shahada).

Kuongeza Sifa Nyingine (Optional)

  • Mafunzo mafupi, kozi, n.k.

Kuona Nafasi za Kazi

  • Zinaonyeshwa kulingana na kiwango cha elimu cha mwombaji.

Kuomba Kazi (Apply for a Job)

  • Kupakia barua ya maombi (PDF ≤ 700KB).
  • Kuchagua kituo cha usaili.
  • Kukubali masharti.
  • Kutuma maombi.

Kuangalia Hali ya Maombi (Application Status)

  • Kupitia Dashboard au email/notisi.
  • Kujua kama umeitwa kwenye usaili au kuteuliwa.

Mwongozo huu unapatikana katika tovuti ya ajira Magereza au Pakua hapa PDF.

Soma zaidi: