Haya hapa Matokeo ya Usaili Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Disemba 2025
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inapenda kuwataarifu wasailiwa wote waliofanya usaili wa mchujo tarehe 13 Disemba 2025 katika kada za:
- Afisa Mauzo na Masoko I
- Afisa Mauzo na Masoko II
kuwa matokeo ya usaili yametoka, na wasailiwa waliofaulu wanatakiwa kuhudhuria usaili wa mahojiano kama ilivyoainishwa hapa chini.
Angalia hapa matokeo ya usaili Air Tanzania
Taarifa Muhimu za Usaili wa Mahojiano ATCL
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mwajiri | Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) |
| Kada | Afisa Mauzo na Masoko I & II |
| Aina ya Usaili | Usaili wa Mahojiano (Oral Interview) |
| Tarehe | 15 Disemba 2025 |
| Muda | Kuanzia saa 2:00 asubuhi |
| Mahali | ATC House – Posta, Makao Makuu ya ATCL |
Vitambulisho Vinavyokubalika Kwenye Usaili
Wasailiwa wanapaswa kufika na kitambulisho halali cha utambuzi kama kilivyoorodheshwa hapa chini:
| Na. | Aina ya Kitambulisho |
|---|---|
| 1 | Kitambulisho cha Taifa (NIDA) |
| 2 | Kitambulisho cha Mpiga Kura |
| 3 | Kitambulisho cha Kazi |
| 4 | Kitambulisho cha Mkaazi |
| 5 | Hati ya Kusafiria (Passport) |
| 6 | Leseni ya Udereva |
Orodha ya Vyeti Vinavyotakiwa (Original Certificates)
Wasailiwa wanatakiwa kuwasilisha vyeti halisi kulingana na sifa zao:
| Kiwango cha Elimu / Taaluma | Cheti Kinachotakiwa |
|---|---|
| Kuzaliwa | Cheti cha Kuzaliwa |
| Kidato cha Nne | Cheti cha Form IV |
| Kidato cha Sita | Cheti cha Form VI |
| Elimu ya Kati | Astashahada / Stashahada |
| Elimu ya Juu | Stashahada ya Juu / Shahada na kuendelea |
| Taaluma Maalum | Cheti cha Usafiri wa Anga (Aviation Certificate) |
Nyaraka Zisizokubalika Kwenye Usaili
Wasailiwa hawataruhusiwa kuendelea na usaili iwapo watawasilisha nyaraka zifuatazo:
- Testimonials
- Provisional Results
- Form IV Result Slips
- Form VI Result Slips
Maelekezo ya Ziada kwa Wasailiwa
- Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi
- Zingatia tarehe, muda na mahali ulipopangiwa kufanyia usaili
- Wasailiwa wenye tofauti ya majina wahakikishe wana Deed Poll iliyosajiliwa
- Waliozaliwa nje ya Tanzania wawasilishe uthibitisho wa uraia kutoka Uhamiaji
Hitimisho
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inawahimiza wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wa mahojiano kufuata maelekezo yote yaliyotolewa ili kuhakikisha usaili unafanyika kwa ufanisi na bila usumbufu.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments