Haya hapa Matokeo ya Udahili Awamu ya Tatu NACTVET 2025 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linauarifu umma kuwa matokeo ya uchaguzi wa awamu ya tatu kwa waombaji wa programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2025/2026 yametangazwa rasmi tarehe 5 Oktoba, 2025.
Baraza limeendesha udahili huo kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System – CAS) kwa vyuo vinavyotoa programu mbalimbali za afya nchini.
Taarifa Muhimu za Matokeo
- Jumla ya waombaji waliokamilisha maombi: 10,622
- Wenye sifa kwenye programu walizoomba: 9,697
- Wasiokuwa na sifa: 925
- Waliochaguliwa kujiunga na vyuo: 6,271
- Wanawake: 3,276 (52%)
- Wanaume: 2,995 (48%)
- Vyuo vya Serikali: 194 waombaji
- Vyuo visivyo vya Serikali: 6,077 waombaji
Maelekezo kwa Waombaji
- Waombaji wote wanaweza kuangalia matokeo yao kupitia tovuti rasmi ya Baraza: www.nactvet.go.tz
Kisha bofya sehemu iliyoandikwa “CAS Selection 2025” kupata matokeo yako. - Waombaji wenye sifa lakini hawakuchaguliwa kutokana na ushindani wanashauriwa kuomba tena katika vyuo vyenye nafasi wazi kupitia dirisha la awamu ya nne.
- Dirisha la awamu ya nne na la mwisho limefunguliwa kuanzia 5 hadi 15 Oktoba, 2025, na matokeo yatatolewa tarehe 21 Oktoba, 2025.
- Kwa waombaji wanaotaka kubadilisha programu au chuo, dirisha la uhamisho (transfer) limefunguliwa katika kipindi hicho hicho (5–15 Oktoba, 2025).
- Uhamisho unafanywa kupitia akaunti binafsi ya mwombaji kwenye mfumo wa CAS.
Wito wa NACTVET kwa Umma
Baraza linawashauri waombaji wote kufuatilia taarifa rasmi kupitia tovuti yake na kuepuka taarifa zisizo sahihi kutoka vyanzo visivyo rasmi. Pia, wanahimizwa kutumia nafasi hii ya mwisho kwa uangalifu ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kuendelea na masomo katika mwaka wa masomo 2025/2026.
Imetolewa na:
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET)
Tarehe: 5 Oktoba, 2025
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments