Tangazo la Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo vya VETA – Muhula wa Masomo Januari 2026
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inapenda kuutangazia umma kuwa uchaguzi wa waombaji kujiunga na elimu na mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vya VETA kwa muhula wa masomo unaoanza Januari 2026 umekamilika kwa awamu ya kwanza.
Bonyeza hapa kupakua PDF ya majina
Awamu ya Pili ya Uchaguzi
Awamu ya pili ya majina ya waliochaguliwa itatangazwa kuanzia tarehe 23 Desemba, 2025.
Joining Instructions (Maelekezo ya Kujiunga)
Orodha ya majina ya waliochaguliwa pamoja na maelekezo ya kujiunga (Joining Instructions) kwa kila chuo:
- Yanapatikana kwenye tovuti rasmi ya VETA: www.veta.go.tz
- Pia yanapatikana katika vyuo vyote vya VETA nchini
Tarehe Muhimu kwa Waliochaguliwa
| Tukio | Tarehe |
|---|---|
| Mwisho wa kufika chuoni | 13 Januari, 2026 |
| Kuanza kwa masomo | 15 Januari, 2026 |
Waliochaguliwa wanatakiwa kufika vyuoni kabla au ifikapo tarehe 13 Januari, 2026.
Mamlaka ya Tangazo
Tangazo hili limetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
UFUNDI STADI, FURSA KAMA ZOTE
Tovuti: www.veta.go.tz
Simu: 0755 267 489
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments