Table of Contents
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza maboresho mapya kwenye Mfumo wa Ajira Portal ili kurahisisha mchakato wa uwasilishaji wa maombi ya kazi kwa waombaji wote.
Uhuishaji wa Taarifa za Elimu
- Waombaji wote ambao tayari wameweka taarifa zao kwenye mfumo wa Ajira Portal wanapaswa kuhuisha taarifa zao za elimu ya Sekondari.
- Waingize Namba ya Mtihani wa Kidato cha Nne (Index Number) katika sehemu ya Academic Qualifications.
- Kwa waliofanya Kidato cha Sita, lazima pia waingize Index Number ya Kidato cha Sita kwenye akaunti zao.
- Hatua hii ni lazima, kwani bila kufanya maboresho haya waombaji hawataweza kuendelea na uwasilishaji wa maombi ya kazi.
Hakuna Tena Wajibu wa Kupakia Vyeti
- Baada ya maboresho haya, waombaji hawatalazimika tena kuingiza nakala za vyeti vya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita.
- Badala yake, Index Number pekee ndiyo itatumika.
- Taarifa za kitaaluma zitachukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye mfumo wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
Waombaji Waliosoma Nje ya Nchi
- Waombaji waliomaliza masomo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita nje ya Tanzania pia watahusika na maboresho haya.
- Watalazimika kutumia namba za equivalence wanazopatiwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) ili kuboresha taarifa zao kwenye mfumo.
Ujazaji wa Taarifa za Kozi
- Eneo la kujaza kozi limeboreshwa.
- Zamani, mtumiaji alilazimika kuchagua category kwanza kisha kozi.
- Sasa, mtumiaji ataweza kutafuta moja kwa moja jina la kozi yake bila kujali ipo katika category ipi, na kisha kuichagua.
Muonekano Mpya wa Ajira Portal
- Mfumo umepata muonekano mpya, wa kisasa na rafiki zaidi.
- Maboresho haya yanalenga hasa wale wanaotumia simu za mkononi ili kuhakikisha urahisi wa kutumia mfumo.
Angalizo Muhimu
Maboresho haya yanahusu mfumo wa Ajira Portal pekee.
- Waombaji watakapoitwa kwenye usaili, watalazimika kufika na vyeti vyao halisi kuanzia Kidato cha Nne na kuendelea.
Tangazo hili pia linapatikana katika tovuti ya Ajira portal Tanzania au pakua PDF yake hapa.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments