Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za ajira kwa mwaka 2025, likiwakaribisha vijana wa Kitanzania wenye sifa na nia ya kulitumikia taifa kupitia jeshi. Tangazo hili linahusisha nafasi kwa askari wa kawaida na maafisa wanaotarajiwa.
Sifa za Waombaji
Ili kujiunga na JWTZ, waombaji wanapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
- Raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 25.
- Elimu ya kidato cha nne au sita, na awe amefaulu.
- Awe hajaoa wala hajaolewa.
- Awe na afya njema ya mwili na akili, na mwenye tabia na mwenendo mzuri.
- Asiwe amewahi kuhukumiwa kwa kosa lolote la jinai.
- Awe amehitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mkataba wa kujitolea wa miaka miwili au kwa mujibu wa sheria, na awe na cheti halisi cha kuhitimu.
Utaratibu wa Maombi
Waombaji wanatakiwa kuwasilisha barua rasmi ya kuomba nafasi, ikieleza dhamira ya kujiunga na jeshi. Barua hiyo iambatane na nakala za cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu, kitambulisho cha taifa (NIDA), na picha ndogo (passport size).
Maombi yote yanapaswa kutumwa kwa anuani ifuatayo:
Tanzania People’s Defence Force (TPDF)
P.O Box 194
Miyuji / Msalato
Dodoma – Tanzania
Mafunzo na Utumishi
Baada ya kuchaguliwa, waombaji wataanza mafunzo ya awali ya kijeshi. Kwa wale wanaotaka kuwa maafisa, wanapaswa kuwa na elimu ya kidato cha sita au zaidi, na watapitia usaili maalum kabla ya kupelekwa katika Chuo cha Kijeshi cha Tanzania (Tanzania Military Academy – TMA) kwa mafunzo ya mwaka mmoja.
Baada ya kufaulu mafunzo, askari hutumikia JWTZ kwa kipindi cha awali cha miaka sita. Baada ya hapo, wanaweza kuendelea kwa mkataba wa miaka miwili miwili, kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.
Tahadhari kwa Waombaji
JWTZ inatoa matangazo rasmi kuhusu fursa za kujiunga kupitia vyombo vya habari na tovuti yake rasmi. Waombaji wanashauriwa kufuatilia taarifa sahihi ili kuepuka utapeli wa kazi.
Kwa taarifa zaidi na maelezo ya kina, tembelea tovuti rasmi ya JWTZ:
Soma zaidi:
Leave a Reply