Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba NECTA 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba NECTA 2025 Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) ni hatua muhimu sana kwa kila mwanafunzi wa darasa la saba nchini Tanzania. Matokeo ya mtihani huu huamua ni shule ipi ya sekondari mwanafunzi ataendelea nayo masomo yake.

Kwa mwaka 2025, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) linatarajiwa kutangaza matokeo haya mwishoni mwa Oktoba au mwanzoni mwa Novemba, mara baada ya kumalizika kwa uhakiki wa alama. Wazazi, walezi, na wanafunzi wanapaswa kujua njia sahihi na rahisi za kuangalia matokeo hayo bila usumbufu.

Vitu vya Muhimu Kabla ya Kuangalia Matokeo

Kabla ya kuanza mchakato, hakikisha unayo taarifa zifuatazo:

  • Namba ya Mtihani: mfano PS0101001.
  • Jina la Shule: kama huna namba ya mtihani, unaweza kutumia jina la shule.
  • Intaneti na kifaa: simu janja au kompyuta yenye mtandao.
  • Subira: siku ya kwanza mara nyingi tovuti ya NECTA hupata msongamano wa watumiaji.

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025

  1. Kupitia Tovuti ya NECTA
  2. Kupitia SMS
    • Kila mwaka NECTA au kampuni za simu hutangaza namba maalum ya kutuma ujumbe mfupi.
    • Tuma namba ya mtihani pokea matokeo papo hapo.
  3. Kupitia Tovuti Shirikishi
    • Magazeti makubwa au tovuti za elimu huchapisha matokeo, lakini chanzo rasmi kinabaki NECTA.

Njia kuu ya kuangalia Matokeo

Njia ya KuangaliaHatua Muhimu
NECTA WebsiteNenda www.necta.go.tz kisha PSLE Results kisha Chagua mkoa, wilaya, shule
SMSTuma namba ya mtihani kwenda namba *152*00#, chagua namba 8 ELIMU kisha namba 2 NECTA. (ikiwa tangazo litatolewa)
Tovuti zingineFuata matangazo kwenye tovuti za elimu na magazeti makubwa

Baada ya Matokeo

Mara matokeo yatakapotoka, NECTA hutoa pia orodha ya wanafunzi waliopangiwa kujiunga na kidato cha kwanza. Ni muhimu kuhifadhi matokeo kwa kupakua au kupiga picha ya skrini. Wazazi wanashauriwa kuanza maandalizi mapema ya vifaa na ada kwa ajili ya shule mpya.

Kwa kuzingatia maelekezo haya, kila mzazi na mwanafunzi ataweza kupata matokeo ya PSLE 2025 kwa urahisi na kwa usahihi.

Soma zaidi: