Ajira Mpya Msaidizi wa Hesabu 126

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la Ajira Mpya Msaidizi wa Hesabu Daraja la II Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 126 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili;

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

KadaIdadi ya NafasiNgazi ya Mshahara
Msaidizi wa Hesabu Daraja la II (Accounts Assistant Grade II)126TGS.B

Sifa za Mwombaji

Kuajiriwa wenye Cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali au Cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA.

Masharti Muhimu

  • Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18–45.
  • Aambatishe:
    • Cheti cha kuzaliwa.
    • CV yenye taarifa binafsi na mawasiliano.
    • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya uraia.
    • Nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.
    • Picha mbili (2) za rangi za passport size.
  • Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi waambatishe vyeti vilivyothibitishwa na TCU/NACTE/NECTA.
  • Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips HAVITAKUBALIWA.
  • Taarifa za kughushi zitapelekea hatua za kisheria.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Barua za maombi (ikiandikwa kwa mkono) ziambatane na vyeti vyote muhimu na zitumwe kwa:

KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.

Mwisho wa kutuma maombi: 29 Oktoba, 2025 saa 9:30 Alasiri.

Tuma maombi hapa

Pakua PDF hapa

Soma zaidi: