Hili hapa tangazo la Ajira Mpya Mhasibu Daraja la II Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 131 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili;
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
| Kada | Idadi ya Nafasi | Ngazi ya Mshahara |
|---|---|---|
| Mhasibu Daraja la II (Accountant Grade II) | 131 | TGS.D |
Sifa za Mwombaji
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Sita wenye shahada ya Uhasibu au Biashara waliojiimarisha kwenye fani ya Uhasibu, au wenye Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Taasisi inayotambuliwa na Serikali, pamoja na cheti cha Taaluma ya Uhasibu CPA (T) au sifa inayolingana inayotambuliwa na NBAA.
Masharti Muhimu
- Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18–45.
- Aambatishe:
- Cheti cha kuzaliwa.
- CV yenye taarifa binafsi na mawasiliano.
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya uraia.
- Nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.
- Picha mbili (2) za rangi za passport size.
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi waambatishe vyeti vilivyothibitishwa na TCU/NACTE/NECTA.
- Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips HAVITAKUBALIWA.
- Taarifa za kughushi zitapelekea hatua za kisheria.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Barua za maombi (ikiandikwa kwa mkono) ziambatane na vyeti vyote muhimu na zitumwe kwa:
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Mwisho wa kutuma maombi: 29 Oktoba, 2025 saa 9:30 Alasiri.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments