Walioitwa kwenye Usaili Oral Tume ya Utumishi wa Mahakama 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hii hapa orodha ya majina ya Walioitwa kwenye Usaili Oral Tume ya Utumishi wa Mahakama 2025 Kufuatia usaili wa hatua ya kwanza wa kada mbalimbali uliofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Desemba, 2025 katika vituo tofauti nchini, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia waombaji wote waliotajwa kwenye tangazo hili kuwa wamechaguliwa kuhudhuria usaili wa ana kwa ana (Oral Interview).

Usaili huu wa hatua ya pili utafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 16 Januari, 2026, kwa mujibu wa tarehe na vituo vilivyoainishwa kwenye orodha ya majina ya wasailiwa iliyoambatishwa na tangazo hili.

Aina ya Usaili

  • Kada ya Mwandishi Mwendesha Ofisi II na Dereva II
    ➝ Wataanza na usaili wa vitendo (Practical Interview)
    ➝ Watakaofaulu ndipo wataendelea na usaili wa ana kwa ana (Oral Interview)

Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa

  • Fika kituo cha usaili ulichopewa, saa 2:00 asubuhi
  • Leta nyaraka halisi (Original Certificates) zifuatazo:
    • Vyeti vya Elimu na Taaluma
    • Cheti cha Kuzaliwa
    • Kitambulisho kimojawapo kinachotambulika na Serikali chenye picha:
      • NIDA
      • Kitambulisho cha Mpiga Kura
      • Hati ya Kusafiria
      • Leseni ya Udereva

Msailiwa atakayefika bila nyaraka husika au kuchelewa hatasailiwa.
Hakikisha unahudhuria kituo ulichopewa pekee.

Bonyeza hapa kuangalia majina ya walioitwa

Kwa Wasioona Majina Yao

Waombaji ambao majina yao hayapo kwenye orodha, watambue kuwa hawakuchaguliwa kuendelea na usaili wa hatua ya pili.

Mawasiliano na Taarifa Zaidi

Soma zaidi: