Hili hapa Tangazo la Fursa za Kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi ya Muda Mfupi (Kupitia Mradi wa YEFFA) Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inaendelea kupokea maombi ya kushiriki mafunzo ya ufundi stadi ya muda mfupi kupitia Mradi wa Ujasiriamali wa Vijana kwa Mustakabali wa Chakula na Kilimo (YEFFA).
Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya VETA, AMSHA, RUATI, TAMA na MiBOS, na unafadhiliwa na AGRA Tanzania. Mafunzo yatatolewa katika vyuo vya VETA vya Kihonda, Manyara, Mpanda na Arusha (Oljjoro).
Bonyeza hapa kuangalia tangazo katika PDF
Kupitia mradi huu, vyuo husika vitatoa mafunzo ya muda mfupi katika fani za Agro-Mechanics, Umwagiliaji (Irrigation) na Teknolojia ya Uhifadhi wa Mazao Baada ya Mavuno (Post-Harvest Technology). Mafunzo yatatolewa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza itaanza tarehe 19 Januari, 2026.
Mafunzo yatakuwa ya kutwa (Day Programme).
Fani Zitakazotolewa VETA
Mafunzo ya ufundi stadi yatatolewa katika fani zifuatazo:
- Ufundi wa Zana za Kilimo (Agro-Mechanics)
- Umwagiliaji (Irrigation)
- Teknolojia ya Kuhifadhi Mazao Baada ya Mavuno (Post-Harvest Technology)
Mikoa Inayostahili Kuomba VETA
Waombaji kutoka mikoa ifuatayo wanahimizwa kuomba:
Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Lindi, Morogoro, Pwani, Ruvuma, Njombe, Iringa, Manyara, Singida, Dodoma, Tabora, Katavi, Kigoma, Rukwa, Mbeya, Songwe na Kagera.
Sifa za Kujiunga VETA
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
- Awe Mtanzania
- Awe na umri wa miaka 15 au zaidi
- Awe na elimu ya msingi au kuendelea
Utaratibu wa Kuomba VETA
Maombi yatafanyika kwa njia zifuatazo:
- Mtandaoni (VETA Online Application) au kupitia tovuti ya VETA: www.veta.go.tz
- Kwa kuchukua fomu (Hardcopy) katika vyuo vya VETA vya Kihonda, Manyara, Mpanda na Arusha (Oljjoro).
Maelekezo Muhimu:
- Fomu zote zitatolewa bure na zitajazwa kwa usahihi.
- Mwombaji anatakiwa kuambatanisha cheti cha kuzaliwa na vyeti vya elimu aliyonayo.
- Fomu iliyojazwa irejeshwe chuoni husika au kutumwa mtandaoni kupitia mfumo wa maombi.
Kipindi cha Maombi VETA
| Tukio | Tarehe |
|---|---|
| Kuanza kupokea fomu | 19 Desemba, 2025 |
| Mwisho wa kupokea maombi | 2 Januari, 2026 |
Ada na Gharama za Mafunzo VETA
- Ada ya mafunzo italipwa na AGRA kupitia Mradi wa YEFFA.
- Mafunzo ni bure kwa waombaji waliokidhi vigezo.
Wanawake na watu wenye mahitaji maalum wanahimizwa sana kuomba.
Mawasiliano VETA
Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi, wasiliana na:
VETA Makao Makuu
Barabara ya VETA, Tambukareli
S.L.P 802, Dodoma
Baruapepe: info@veta.go.tz | pr@veta.go.tz
Simu: 0755 26 74 89.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments