Kama umekuwa ukisubiri majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2026 na unataka kujua shule ambayo mtoto wako amepangiwa, basi huu ni mwongozo rahisi utakao kusaidia kufahamu namna ya kuangalia majina, kuelewa mfumo wa upangaji, na kupakua “joining instructions” za TAMISEMI.
Angalia hapa majina waliochaguliwa form one 2026
Form One Selection ni nini?
Form One Selection ni mchakato wa kitaifa unaofanywa kila mwaka na Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Baada ya kutolewa kwa Matokeo ya Darasa la Saba (PSLE) kutoka NECTA, wanafunzi hupangiwa shule za sekondari za Serikali kulingana na:
- Matokeo yao ya PSLE
- Nafasi zilizopo katika shule
- Shule walizozichagua
- Vipaumbele vya mkoa husika
Lengo la TAMISEMI ni kuhakikisha kila mwanafunzi anapata shule kwa usawa na shule zote zinakuwa na uwiano mzuri wa wanafunzi kulingana na uwezo wake.
Matokeo ya Form One Selection 2025 Hutoka Lini?
Baada ya NECTA kutangaza matokeo ya Darasa la Saba, TAMISEMI hufuata na kutoa orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza. Kwa kawaida hutolewa mapema tu baada ya matokeo.
Katika tangazo, utaona:
- Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kwa kila mkoa
- Shule walizopangiwa
- Tarehe muhimu za kufika shuleni
- Joining instructions za kila shule
Namna ya Kuangalia Form One Selection 2025 (Hatua kwa Hatua)
Fuata hatua hizi rahisi:
- Fungua tovuti rasmi ya TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz
- Tafuta tangazo linaloandikwa “Form One Selection 2026”
- Chagua Mkoa
- Chagua Wilaya
- Fungua orodha uone jina la mwanafunzi
- Pakua joining instructions ya shule aliyopangiwa
Jinsi ya Kupakua Joining Instructions za Form One 2026
Baada ya kuthibitisha shule, hakikisha unapakua joining instruction ambazo zina maelezo ya:
- Mahitaji ya mwanafunzi (vifaa muhimu)
- Tarehe ya kuripoti
- Mavazi/uniform na maelekezo ya ada (kama yapo)
- Mawasiliano ya shule
Unaweza kuzipata moja kwa moja kupitia tovuti ya TAMISEMI au katika ukurasa wa shule husika.
Tovuti Rasmi za Kuangalia Form One Selection 2026
- TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz
- NECTA (kwa kumbukumbu za PSLE): www.necta.go.tz
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments