Karibu, Huu hapa ni mwongozo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Tunafurahi kwamba umechagua kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa masomo yako ya juu. Mwongozo huu unakupa muhtasari wa kozi, huduma na maisha ya kila siku kwenye kampasi zetu mbalimbali.
Maisha na Mazingira ya Kujifunzia UDSM
UDSM ni jumuiya ya kipekee ya wanafunzi na wahadhiri. Kila mmoja anajituma ili kuhakikisha unapata uzoefu bora. Kwa sababu hiyo, tunatoa mazingira mazuri ya ufundishaji, ujifunzaji, utafiti na huduma kwa jamii.
Chuo kimejenga sifa kubwa ndani na nje ya Afrika. Zaidi ya hapo, tumekuwa tukiboresha miundombinu ya kujifunzia ili kuhakikisha unapata elimu inayokidhi mahitaji ya dunia ya sasa.
Tunahakikisha kipindi utakachokaa hapa kinafurahisha na kukupa kumbukumbu nzuri. Pia, tunatambua kuwa maisha ya chuo hayahusu masomo pekee. Hivyo, tunawahimiza wanafunzi washiriki kwenye shughuli za DARUSO pamoja na michezo kama kuogelea, riadha, mpira wa miguu na kriketi.
Ubunifu, Uvumbuzi na Uongozi wa Kitaaluma
UDSM inaendelea kuongoza katika mageuzi ya elimu ya juu nchini na kimataifa. Chuo kimehakikisha taarifa zote kwenye mwongozo huu kuhusu kozi, muundo, wahadhiri na miundombinu ni sahihi.
Hata hivyo, kutokana na changamoto za kiutendaji, si kila kozi ya uchaguzi inaweza kutolewa kila mwaka wa masomo.
Msaada na Ushauri kwa Wanafunzi
Tunatumaini mwongozo huu utakusaidia kupata taarifa unazohitaji. Iwapo hautapata maelezo fulani, unaweza kuwasiliana na Kurugenzi ya Masomo ya Shahada ya Kwanza kwa msaada wa ziada.
Mara nyingine tena, tunakukaribisha sana UDSM. Tunatazamia kushirikiana nawe katika kutimiza malengo yako ya kitaaluma. Maeleo haya yote unaweza yapata kupitia tovuti ya Chuo hapa https://www.udsm.ac.tz
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments