Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi sita (06) za kazi katika Manispaa hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:-
Mwisho wa kutuma maombi: 27 Novemba 2025
Njia ya kutuma maombi: Kupitia Recruitment Portal https://portal.ajira.go.tz
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
| Nafasi | Idadi | Sifa za Mwombaji | Mshahara |
|---|---|---|---|
| Dereva wa Mitambo Daraja II | 2 | Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja ‘G’ ya uendeshaji mitambo pamoja na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo hiyo, wenye uzoefu wa kuendesha mitambo (GREDA) kwa muda usiopungua saa mia tatu (300) au miezi mitatu (3) bila kusababisha ajali. | TGOS A |
| Dereva Daraja II | 4 | Kidato cha IV/VI, Leseni ya Daraja C au E, Cheti cha Udereva kutoka VETA/Chuo kinachotambuliwa na Serikali, uzoefu angalau mwaka 1 bila ajali | TGS B |
Masharti ya Jumla
- Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri miaka 18–45.
- Waambatishe cheti cha kuzaliwa, CV yenye anuani, simu na wadhamini 3.
- Vyeti vya taaluma lazima viwe vimethibitishwa na Mwanasheria.
- Vyeti vya provisional, statement of results na result slips HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na NECTA/NACTVET/TCU.
- Waombaji wa kazi ya Dereva lazima waambatishe vyeti vya udereva vinavyoonesha sifa za kupata daraja husika.
- Waliostaafu Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Maombi yaandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia Recruitment Portal.
Jinsi ya kutuma maombi
Maombi yote yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal):
https://portal.ajira.go.tz
Barua ya maombi ielekezwe kwa:
Mkurugenzi wa Manispaa,
Manispaa ya Iringa,
S.L.P 162,
IRINGA
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments