Nafasi za Kazi Mwalimu Daraja la III B Hisabati 709

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la Ajira Mpya Mwalimu Daraja la III B Hisabati 709 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 709 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili;

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

KadaIdadi ya NafasiNgazi ya Mshahara
Mwalimu Daraja la III B – Hisabati (Mathematics)709TGS.B

Sifa za Mwombaji

Kuajiriwa mwenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la Hisabati kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.

Masharti Muhimu

  • Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18–45.
  • Aambatishe:
    • Cheti cha kuzaliwa.
    • CV yenye taarifa binafsi na mawasiliano.
    • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya uraia.
    • Nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.
    • Picha mbili (2) za rangi za passport size.
  • Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi waambatishe vyeti vilivyothibitishwa na TCU/NACTE/NECTA.
  • Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips HAVITAKUBALIWA.
  • Taarifa za kughushi zitapelekea hatua za kisheria.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Barua za maombi (ikiandikwa kwa mkono) ziambatane na vyeti vyote muhimu na zitumwe kwa:

KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.

Mwisho wa kutuma maombi: 01 Novemba, 2025 saa 9:30 Alasiri.

Pakua PDF hapa

Soma zaidi: