Hili hapa tangazo la Ajira Mpya Msaidizi wa Hesabu Daraja la II Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 126 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili;
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
| Kada | Idadi ya Nafasi | Ngazi ya Mshahara |
|---|---|---|
| Msaidizi wa Hesabu Daraja la II (Accounts Assistant Grade II) | 126 | TGS.B |
Sifa za Mwombaji
Kuajiriwa wenye Cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali au Cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA.
Masharti Muhimu
- Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18–45.
- Aambatishe:
- Cheti cha kuzaliwa.
- CV yenye taarifa binafsi na mawasiliano.
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya uraia.
- Nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.
- Picha mbili (2) za rangi za passport size.
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi waambatishe vyeti vilivyothibitishwa na TCU/NACTE/NECTA.
- Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips HAVITAKUBALIWA.
- Taarifa za kughushi zitapelekea hatua za kisheria.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Barua za maombi (ikiandikwa kwa mkono) ziambatane na vyeti vyote muhimu na zitumwe kwa:
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Mwisho wa kutuma maombi: 29 Oktoba, 2025 saa 9:30 Alasiri.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments