Hili hapa tangazo la ajira mpya Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 17,710 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili;
Ajira Mpya zilizotangazwa na Maelezo
| Kada | Idadi ya Nafasi | Sifa za Mwombaji (Muhtasari) | Mshahara |
|---|---|---|---|
| Mhassibu Daraja la II | 131 | Shahada ya Uhasibu/CPA(T) au Stashahada ya juu ya Uhasibu kutoka taasisi inayotambuliwa na Serikali | TGS.D |
| Afisa Uvuvi Msaidizi II | 35 | Diploma ya Sayansi ya Uvuvi au fani inayofanana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali | TGS.C |
| Dereva Daraja la II | 427 | Kidato cha Nne, leseni daraja C/E, uzoefu wa mwaka 1, mafunzo ya VETA | TGOS.A |
| Afisa Hesabu Daraja la II | 224 | Kuajiriwa wenye “Intermidiet Certificate” (Module D) inayotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA | TGS.D |
Kuona nafasi za kazi 17710 MDAs & LGAs endelea kusoma na download PDF hapo chini.
Masharti Muhimu
- Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18–45.
- Aambatishe:
- Cheti cha kuzaliwa.
- CV yenye taarifa binafsi na mawasiliano.
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya uraia.
- Nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.
- Picha mbili (2) za rangi za passport size.
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi waambatishe vyeti vilivyothibitishwa na TCU/NACTE/NECTA.
- Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips HAVITAKUBALIWA.
- Taarifa za kughushi zitapelekea hatua za kisheria.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Barua za maombi (ikiandikwa kwa mkono) ziambatane na vyeti vyote muhimu na zitumwe kwa:
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Mwisho wa kutuma maombi: 29 Oktoba, 2025 saa 9:30 Alasiri.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments