Table of Contents
Hili hapa tangazo la nafasi za lazo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za ajira mpya baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
| Kada | Idadi ya Nafasi | Majukumu Makuu | Sifa za Mwombaji | Ngazi ya Mshahara |
|---|---|---|---|---|
| Dereva Daraja la II | 6 | – Kukagua gari kabla na baada ya safari kuhakikisha usalama. – Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi na kufanya matengenezo madogo ya gari. | – Awe na cheti cha Kidato cha Nne (Form IV). – Awe na Leseni ya Daraja E au C yenye uzoefu wa angalau mwaka 1 bila ajali. – Awe amehitimu Mafunzo ya Msingi ya Udereva (Basic Driving Course) kutoka VETA au chuo kinachotambulika na Serikali. | TGS B1 |
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Mwombaji awe Raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
- Aambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na wakili au mwanasheria.
- Awe na maelezo binafsi (CV) yenye anuani, namba za simu, barua pepe, na wadhamini watatu.
- Aambatishe vyeti halisi vilivyothibitishwa vya taaluma na elimu.
- Matokeo (Result Slips), Testimonials, Statement of Results hazitakubaliwa.
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi wahakikishe vyeti vimeidhinishwa na TCU, NECTA au NACTE.
- Wastaafu hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waajiriwa wa Serikali wasiombe kwa nafasi za kuingilia moja kwa moja.
- Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kutuma maombi na kuainisha aina ya ulemavu.
- Wenye majina tofauti kwenye vyeti wawasilishe Hati ya Kiapo (Deed Poll).
- Maombi yenye taarifa za kughushi yatatupiliwa mbali na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
- Waombaji wanaoitwa kwenye usaili wanashauriwa kuvaa mavazi yanayozuia baridi kwa kuzingatia hali ya hewa ya Arusha.
Namna ya Kutuma Maombi
- Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa Recruitment Portal: https://portal.ajira.go.tz
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”) - Barua za maombi ziandikwe kwa jina la:
Mkurugenzi wa Jiji,
Halmashauri ya Jiji la Arusha,
S.L.P. 3013, 20 Barabara ya Boma, 23101 ARUSHA.
Mwisho wa Kutuma Maombi
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 20 Oktoba, 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments