Hii hapa orodha ya majina ya Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Awamu ya Pili TCU 2025 kujiunga na chuo Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kuufahamisha umma, Taasisi za Elimu ya Juu na wadau wa elimu kuwa Awamu ya Kwanza ya Udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026 imekamilika.
Majina ya waliodahiliwa katika awamu hii yanatangazwa na vyuo husika.
Takwimu Muhimu za Awamu ya Kwanza
Kipengele | Mwaka 2024/2025 | Mwaka 2025/2026 | Tofauti / Ongezeko |
---|---|---|---|
Idadi ya vyuo vilivyoshiriki udahili | 86 | 88 | +2 |
Idadi ya programu zilizoidhinishwa | 856 | 894 | +38 |
Idadi ya nafasi za udahili | 198,986 | 205,652 | +6,666 (3.3%) |
Idadi ya waombaji wote | 142,300 (takriban) | 146,879 | +4,579 |
Waliopata udahili | 113,400 | 116,596 | +3,196 |
Asilimia ya waliopata udahili | 79.7% | 79.4% | -0.3% |
Waombaji Waliodahiliwa Katika Chuo Zaidi ya Kimoja
Waombaji waliodahiliwa katika zaidi ya chuo kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kati ya tarehe 03 hadi 21 Septemba, 2025.
Uthibitisho unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri (confirmation code) iliyotumwa kwa ujumbe mfupi (SMS) au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.
Kwa wale ambao hawajapokea ujumbe huo kwa wakati, wanashauriwa:
- Kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa, na
- Kuomba kutumiwa namba ya siri upya.
Uthibitisho unapaswa kufanyika kupitia akaunti binafsi ya mwombaji.
Orodha ya majina ya waliodahiliwa katika zaidi ya chuo kimoja inapatikana kwenye tovuti ya TCU: www.tcu.go.tz
Kuanza kwa Awamu ya Tatu ya Udahili
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inatangaza rasmi kuanza kwa Awamu ya Pili ya Udahili wa Shahada ya Kwanza kuanzia tarehe 06 Octoba na kuendelea
Waombaji ambao:
- Hawakutuma maombi ya udahili katika Awamu ya Kwanza; au
- Hawakupata nafasi ya kudahiliwa,
wanahimizwa kutumia fursa hii kwa kutuma maombi kwenye vyuo wanavyopendelea.
Vyuo vya Elimu ya Juu vinaelekezwa kutangaza programu ambazo bado zina nafasi wazi, na waombaji wanatakiwa kuzingatia kalenda ya udahili iliyoko kwenye tovuti ya TCU.
Wito kwa Waombaji
Waombaji wanakumbushwa kuwa:
- Masuala yote yahusuyo udahili au uthibitisho yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.
- Vyuo vimeelekezwa kushughulikia changamoto za uthibitisho kwa haraka na kwa mujibu wa miongozo ya TCU.
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
Jengo la SUMA JKT, S.L.P. 2600, 1 Mtaa wa JKT, 4110 Tambukareli, Dodoma
Simu: +255 22 2113694 / 2113691
Barua pepe: es@tcu.go.tz
Tovuti: www.tcu.go.tz
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments