Nafasi za Kazi Wilaya ya Kisarawe

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

NafasiIdadiMajukumu MakuuSifa za MwombajiNgazi ya Mshahara
Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (Office Management Secretary)03– Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri. – Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao kisha kuwaelekeza sehemu husika.– Kidato cha IV au VI. – Stashahada (Diploma) ya Uhazili au NTA Level 6. – Uwezo wa hatimkato maneno 100 kwa dakika (Kiswahili na Kiingereza). – Mafunzo ya kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email na Publisher).TGS C

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  1. Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45.
  2. Wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na waainishe aina ya ulemavu.
  3. Waambatanishe CV yenye maelezo ya msingi, anuani, barua pepe na majina ya wadhamini watatu (referees).
  4. Vyeti vya elimu na taaluma viwe vimethibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  5. Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na result slips za kidato cha IV na VI hazitakubaliwa.
  6. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTVET.
  7. Waliostaafu au walioajiriwa tayari katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba (isipokuwa wenye kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi).
  8. Waliowasilisha taarifa au vyeti vya kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
  9. Waombaji wenye majina tofauti katika nyaraka zao wambatanishe Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll).

Jinsi ya Kutuma Maombi

  • Maombi yote yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal): https://portal.ajira.go.tz
  • Mwisho wa kutuma maombi ni 12 Oktoba 2025.
  • Barua ya maombi ielekezwe kwa:

Pakua PDF hapa.

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe
S.L.P 28001
Kisarawe

Soma zaidi: