Nafasi za Kazi Mkataba Wilaya ya Mlimba

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba imepata mradi wa FOLUR unaofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) chini ya usimamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Kupitia mradi huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba anatangaza nafasi za ajira za mkataba kwa Watanzania wenye sifa kama ifuatavyo:

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

NafasiIdadiMasharti ya AjiraMshahara
Afisa Ugani (Field Extension Officer)2Mkataba wa mwaka 1 unaoweza kuhuishwa hadi miaka 4Kwa mujibu wa taratibu za mradi

Sifa za Mwombaji

  • Shahada (Bachelor’s degree) katika moja ya fani: Kilimo, Maliasili, Ardhi, Mazingira, Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya Jamii.
  • Uzoefu wa angalau miaka 3 katika kupanga, kutekeleza miradi na kuhamasisha jamii.
  • Kipaumbele kwa waliowahi kushiriki miradi ya usimamizi wa maliasili kupitia Serikali au NGOs.
  • Uelewa wa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.
  • Ujuzi wa uongozi, mawasiliano, ushirikishaji na mahusiano ya kijamii.
  • Uwezo wa kushirikiana na viongozi wa kimila, jamii na maafisa wa Serikali.
  • Uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.
  • Awe na leseni halali ya udereva na uwezo wa kuendesha pikipiki.

Majukumu Makuu

  • Kuratibu mikutano na semina za jamii na wadau.
  • Kusaidia utekelezaji wa shughuli za mradi kuhusu matumizi endelevu ya misitu, maji na ardhi.
  • Kushirikiana na jamii, viongozi wa kimila na Serikali katika utekelezaji.
  • Kushirikiana na Mratibu wa Kongani kuandaa mbinu na mipango ya utekelezaji.
  • Kuratibu na kusaidia maafisa ugani na washirika wa mradi.
  • Kurekodi na kuripoti maendeleo ya shughuli za mradi (nusu mwaka na mwaka).
  • Kuwezesha ufuatiliaji wa mradi (Results Framework na Work Plan Tracking).
  • Kushiriki katika vikao vya menejimenti na warsha za tathmini ya mwaka.
  • Kutoa msaada wa vifaa na ushauri wa kitaalamu.
  • Kushughulikia malalamiko ya jamii na kazi nyingine utakazopangiwa.

Masharti Muhimu

  • Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18–45.
  • Aambatishe:
    • Cheti cha kuzaliwa.
    • CV yenye taarifa binafsi na mawasiliano.
    • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya uraia.
    • Nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.
    • Picha mbili (2) za rangi za passport size.
  • Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi waambatishe vyeti vilivyothibitishwa na TCU/NACTE/NECTA.
  • Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips HAVITAKUBALIWA.
  • Taarifa za kughushi zitapelekea hatua za kisheria.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Barua za maombi (ikiandikwa kwa mkono) ziambatane na vyeti vyote muhimu na zitumwe kwa:

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba
S.L.P 263
IFAKARA

Mwisho wa kutuma maombi: 10 Oktoba, 2025 saa 9:30 Alasiri.

Pakua PDF hapa

Soma zaidi: