Nafasi za Kazi Mji Rufiji 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mji Rufiji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Rufiji anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi kwa kada mbili (02) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

KadaIdadi ya NafasiSifa za MwombajiNgazi ya Mshahara
Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II(Office Management Secretary II)06– Kidato cha IV au VI- Diploma/Uhazili NTA Level 6- Ujuzi wa Hatimkato (Kiswahili & Kiingereza – maneno 100/dakika)- Mafunzo ya Kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher) kutoka chuo kinachotambulika na SerikaliTGS C
Dereva Daraja II(Driver II)04– Kidato cha IV- Leseni Daraja E au C- Uzoefu wa angalau mwaka 1 bila ajali- Vyeti vya Mafunzo ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambulika na SerikaliTGS B

Masharti ya Jumla

  1. Awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18–45.
  2. Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na waainishe ulemavu wao.
  3. Wasilisha C.V yenye mawasiliano sahihi na wadhamini watatu wa kuaminika.
  4. Vyeti vya elimu na taaluma vihalalishwe na Mwanasheria/Wakili.
  5. Vyeti vya nje vihalalishwe na TCU, NECTA au NACTVET.
  6. Wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yatatumwa kupitia mfumo wa kielektroniki: https://portal.ajira.go.tz.

Mwisho wa kutuma maombi: 08 Oktoba, 2025.

Soma zaidi: