Mwongozo wa Kudhibiti UKIMWI

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Mwongozo wa Kudhibiti UKIMWI katika Utumishi wa Umma wa mwaka 2007 ulieleza umuhimu wa kuhuishwa ili kuendana na mahitaji mapya na mabadiliko ya kiafya. Uandaaji wa mwongozo huu mpya unalenga kulinda na kuimarisha afya za watumishi wa Umma ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Changamoto Zilizobainika

Utekelezaji wa mwongozo wa mwaka 2007 ulionesha kuibuka kwa changamoto nyingine kubwa:

  • Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa (MSY) yamekuwa tatizo linalokua miongoni mwa watumishi wa Umma.
  • Magonjwa haya yamesababisha kupungua kwa ufanisi wa kazi na kuongeza gharama za Serikali katika huduma za afya.

Baadhi ya Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa (MSY):

  • Shinikizo kubwa la damu
  • Kisukari
  • Saratani
  • Magonjwa ya njia ya hewa
  • Msongo wa mawazo

Sababu kuu: Mtindo wa maisha usiofaa.

Athari za VVU/UKIMWI na MSY katika Sekta ya Umma

  • Kupotea kwa nguvu kazi.
  • Mahudhurio hafifu kazini.
  • Kupungua kwa ufanisi wa watumishi.
  • Kuongezeka kwa mzigo wa kazi kwa watumishi wengine.
  • Kuongezeka kwa matumizi ya Serikali katika kuwahudumia wagonjwa.

Mikakati ya Taifa:

Juhudi za kudhibiti VVU, UKIMWI na MSY zimejikita katika:

  1. Mkakati wa Taifa wa MSY (2009 – 2015).
  2. Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kisekta wa Kudhibiti VVU na UKIMWI (2013 – 2017).

Afua Zinazotekelezwa:

  • Uimarishaji wa afya na kinga.
  • Elimu na uelewa sahihi kuhusu lishe bora.
  • Uangalizi wa karibu na huduma za matibabu.
  • Mazingira wezeshi ya kufanya kazi.
  • Huduma na msaada kwa wanaoishi na VVU/UKIMWI na MSY.

Wajibu wa Sekta ya Umma:

Sekta ya Umma ina jukumu la:

  1. Kuwezesha watumishi kujikinga na maambukizo ya VVU na UKIMWI na pia kujiepusha na MSY.
  2. Kuwasaidia watumishi wanaoishi na VVU/UKIMWI na MSY ili waweze kuendelea kutoa mchango wao katika kazi.

Soma zaidi: