Hii hapa orodha ya majina ya waliochaguliwa chuo cha Mbeya University of Science and Technology (MUST) inapenda kuwataarifu waombaji wote kuwa, Makamu Mkuu wa Chuo ametangaza orodha ya wanafunzi walioteuliwa kujiunga na programu mbalimbali za Stashahada (Diploma) chini ya ufadhili wa Serikali kwa mwaka wa masomo 2025/2026.
Mbeya University of Science and Technology (MUST) ni matokeo ya mabadiliko ya Mbeya Institute of Science and Technology (MIST) yaliyofanyika kupitia Universities Act No. 7 (2005) pamoja na Mbeya University of Science and Technology Charter, 2013.
Kwa mujibu wa Sheria ya Vyuo Vikuu, kila chuo kikuu kinapaswa kuandaa Katiba (Charter) na kuidhinishwa ili kuruhusiwa kutoa elimu ya chuo kikuu.
Kozi Zinazotolewa
MUST inatoa kozi mbalimbali za muda mrefu kwa ngazi tofauti za elimu kwa Watanzania na wasio Watanzania wenye sifa za kujiunga. Ngazi hizo ni:
- Astashahada (Certificates)
- Stashahada (Diploma)
- Shahada za Kwanza (Bachelor Degrees)
- Stashahada ya Uzamivu katika Elimu ya Ufundi (Postgraduate Diploma in Technical Education)
- Shahada za Uzamili (Masters Degrees)
- Shahada za Uzamivu (Doctor of Philosophy – PhD)
Tarehe ya Kuripoti
Wanafunzi wote walioteuliwa wanapaswa kuripoti chuoni kwa ajili ya usajili na mafunzo ya utambulisho kuanzia 25 Oktoba, 2025.
Maelekezo Muhimu (Joining Instructions)
Wanafunzi wote wanatakiwa kupakua na kusoma maelekezo ya kujiunga (Joining Instructions) kupitia tovuti rasmi ya Chuo:
www.must.ac.tz
Salamu za Pongezi
MUST inawapongeza wanafunzi wote waliopata nafasi za masomo na kuwakaribisha kwa dhati kujiunga na familia ya Chuo kwa safari ya taaluma na maendeleo ya kitaaluma.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments