Matokeo ya Waliochaguliwa Vyuo Katika Udahili wa Kwanza NACTVET 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Haya hapa matokeo na orodha ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya kati udahili Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautaarifu umma kuwa matokeo ya awamu ya kwanza ya uhakiki wa waombaji waliochaguliwa kujiunga na programu mbalimbali kwa mkupuo wa Septemba 2025/2026 katika ngazi ya Astashahada na Stashahada yametolewa rasmi leo, 14 Agosti 2025.

Takwimu za Uhakiki

  • Jumla ya waombaji waliowasilishwa: 43,042
    • Wanawake: 22,109 (51%)
    • Wanaume: 20,933 (49%)
  • Waombaji waliokidhi vigezo: 41,839 (97%)
    • Wanawake: 21,557
    • Wanaume: 20,282
  • Waombaji wasio na sifa: 1,203 (3%)

Namna ya Kupata Matokeo

Waombaji wote wanaweza kuona taarifa zao za uhakiki kwa:

  1. Kutumia msimbo maalum uliotumwa kwenye namba ya simu na barua pepe wakati wa kuwasilisha taarifa.
  2. Kubonyeza kitufe cha “Uhakiki Muhula wa Septemba 2025” kupitia tovuti ya Baraza: www.nactvet.go.tz.

Kumbuka: Msimbo huo utatumika pia katika usajili wakati wa kuripoti chuoni.

Dirisha la Awamu ya Pili

Baraza limefungua dirisha la udahili wa awamu ya pili kuanzia 14 Agosti hadi 18 Septemba 2025.

Soma zaidi: