Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Kwa niaba ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) inakaribisha waombaji kazi wa Tanzania wenye sifa stahiki na uwezo wa kujituma kuomba nafasi (20) zilizotajwa hapa chini.
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ilianzishwa chini ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania CAP 51 kama chombo cha serikali kinachojitegemea kwa kiasi, chini ya Wizara ya Kilimo.
TARI ina jukumu la kufanya, kukuza, kudhibiti na kuratibu shughuli zote za utafiti wa kilimo Tanzania Bara.
Taasisi inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki kwa ajili ya nafasi zifuatazo:
Ajira zilizotangazwa na Maelezo
Na. | Nafasi ya Kazi | Idadi ya Nafasi | Mwajiri |
---|---|---|---|
1 | Plant Operator Grade II | 5 | TARI |
2 | Laboratory Technician Grade II (Laboratory Technology) | 5 | TARI |
3 | Research Assistant (Horticulture) | 2 | TARI |
4 | Research Assistant (Agronomy) | 2 | TARI |
5 | Research Assistant (Biotechnology) | 4 | TARI |
6 | Research Assistant (Soil Science) | 2 | TARI |
Masharti ya Jumla ya Maombi:
- Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja hali yao wazi kwenye mfumo wa maombi.
- Ambatanisha CV yenye taarifa sahihi za mawasiliano, anwani, barua pepe na simu.
- Maombi yaambatanishwe na nakala zilizohakikiwa za vyeti vya kitaaluma (Postgraduate, Shahada, Diploma, Cheti), matokeo ya kitaaluma, vyeti vya kidato cha IV na VI, vyeti vya usajili (kama inahitajika), na cheti cha kuzaliwa.
- Haikubaliki kuambatanisha results slips, testimonials au partial transcripts.
- Weka pasipoti-size picha ya hivi karibuni kwenye mfumo wa maombi.
- Watumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
- Wastaafu wa utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
- Taja waamuzi watatu (referees) wenye mawasiliano sahihi.
- Vyeti vya shule vilivyotolewa nje ya nchi vihakikiwe na NECTA; vyeti vya kitaaluma vihakikiwe na TCU au NACTE.
- Barua ya maombi iwe na sahihi, iandikwe Kiswahili au Kiingereza
- Walioteuliwa tu ndio watajulishwa tarehe ya usaili.
- Nyaraka au taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
Jinsi ya kutuma maombi
Maombi yote yatumiwe kupitia Recruitment Portal: http://portal.ajira.go.tz/ (pia inapatikana kupitia tovuti ya PSRS kwa kubofya Recruitment Portal).
Mwisho wa kupokea maombi: 24 Agosti 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments