Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Kwa niaba ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) inakaribisha waombaji kazi wa Tanzania wenye sifa stahiki na uwezo wa kujituma kuomba nafasi (05) zilizotajwa hapa chini.
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA)
TEMESA ilianzishwa tarehe 26 Agosti 2005 chini ya Executive Agencies Act No. 30 of 1997 kupitia Tangazo la Serikali Na. 254. Lengo lake ni kutoa huduma bora na za haraka za umeme, mitambo na elektroniki, huduma salama na za uhakika za usafiri wa vivuko, pamoja na kukodisha vifaa kwa taasisi za serikali na wananchi kwa ujumla.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
Nafasi | Idadi | Mwajiri | Tarehe ya Mwisho Kutuma Maombi |
---|---|---|---|
Diver Daraja la II | 5 | TEMESA | 22 Agosti 2025 |
Masharti ya Jumla ya Maombi:
- Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja hali yao wazi kwenye mfumo wa maombi.
- Ambatanisha CV yenye taarifa sahihi za mawasiliano, anwani, barua pepe na simu.
- Maombi yaambatanishwe na nakala zilizohakikiwa za vyeti vya kitaaluma (Postgraduate, Shahada, Diploma, Cheti), matokeo ya kitaaluma, vyeti vya kidato cha IV na VI, vyeti vya usajili (kama inahitajika), na cheti cha kuzaliwa.
- Haikubaliki kuambatanisha results slips, testimonials au partial transcripts.
- Weka pasipoti-size picha ya hivi karibuni kwenye mfumo wa maombi.
- Watumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
- Wastaafu wa utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
- Taja waamuzi watatu (referees) wenye mawasiliano sahihi.
- Vyeti vya shule vilivyotolewa nje ya nchi vihakikiwe na NECTA; vyeti vya kitaaluma vihakikiwe na TCU au NACTE.
- Barua ya maombi iwe na sahihi, iandikwe Kiswahili au Kiingereza
- Walioteuliwa tu ndio watajulishwa tarehe ya usaili.
- Nyaraka au taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
Jinsi ya kutuma maombi
Maombi yote yatumiwe kupitia Recruitment Portal: http://portal.ajira.go.tz/ (pia inapatikana kupitia tovuti ya PSRS kwa kubofya Recruitment Portal).
Mwisho wa kupokea maombi: 22 Agosti 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments