Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kwa ajili ya ajira mpya ya mwaka wa fedha 2024/2025 kama ilivyoidhinishwa na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
1. Dereva Daraja la II – Nafasi 3
Sifa:
- Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV)
- Leseni ya Daraja E au C
- Uzoefu wa angalau mwaka 1 bila kusababisha ajali
- Cheti cha mafunzo ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali
Mshahara: TGS B
Majukumu: Kukagua gari, kuendesha kwa safari za kikazi, kufanya matengenezo madogo, na kazi nyingine za udereva
2. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 3
Sifa:
- Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI)
- Stashahada (NTA Level 6) ya utunzaji wa kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa
- Ujuzi wa kutumia kompyuta
Mshahara: TGS C
Majukumu: Kuorodhesha barua, kusambaza majalada, kufuatilia mzunguko wa majalada n.k.
Maelekezo kwa Waombaji:
Awe Mtanzania mwenye umri kati ya miaka 18 – 45
Ambatanisha:
- Barua ya maombi (iliyosainiwa)
- Vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili
- CV yenye maelezo kamili, namba za simu, email, na majina ya wadhamini 3
- Epuka kuambatisha: Statement of Results, Provisional Results, Result Slip
- Vyeti vya nje ya nchi vihakikiwe na NECTA/NACTE/TCU
- Ajira hizi si kwa waliostaafu au walioko kwenye ajira ya kuingilia Serikalini
- Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria
Jinsi ya kutuma maombi
Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa Ajira Serikalini:
https://portal.ajira.go.tz
Anuani ya barua iandikwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
S.L.P 18, MALINYI
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments