Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kwa ajili ya ajira mbadala ya mwaka wa fedha 2024/2025 kama ilivyoidhinishwa na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
1. Dereva Daraja la II – Nafasi 6
Sifa za Mwombaji:
- Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV)
- Leseni ya daraja E au C
- Uzoefu wa kuendesha kwa mwaka 1 au zaidi bila kusababisha ajali
- Cheti cha mafunzo ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambulika na Serikali
Majukumu ya Kazi:
- Kukagua usalama wa gari kabla na baada ya safari
- Kuwasafirisha watumishi kwa safari za kikazi
Mshahara:
Kwa mujibu wa viwango vya serikali – TGS B
Maelekezo Muhimu kwa Waombaji:
- Umri: Miaka 18 hadi 45
- Uambatishe:
- Barua ya maombi (iliyosainiwa)
- Vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili
- CV yenye maelezo kamili, simu, email na wadhamini 3
- Cheti cha mafunzo ya udereva
- Hakikisha huambatishi: Statement of Results, Results Slip, au Provisional Results
- Ikiwa ulisoma nje ya nchi, hakikisha vyeti vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTE
- Wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali maalum
- Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja aina ya ulemavu wao
Jinsi ya kutuma maombi
Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal):
https://portal.ajira.go.tz
Anuani ya barua iandikwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Momba
S.L.P 273, MOMBA
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments