Nafasi za Kazi Mji wa Babati

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati amepata kibali cha ajira kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kupitia barua yenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/A/25 ya tarehe 29/04/2025 kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Anaalika Watanzania wenye sifa kuomba nafasi zifuatazo:

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

1. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II – Nafasi 3

Majukumu ya Kazi:

  • Kuchapa barua na nyaraka za kawaida na siri
  • Kupokea wageni na kuelekeza wanapopaswa kwenda
  • Kutunza kumbukumbu, ratiba na miadi ya mkuu wake
  • Kusimamia majalada na nyaraka za idara
  • Kuandaa dondoo, vifaa na maandalizi ya vikao

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya Kidato cha IV au VI
  • Stashahada (Diploma) ya Uhazili au NTA Level 6 ya Uhazili
  • Uwezo wa kuchapa maneno 100 kwa dakika kwa Kiswahili na Kiingereza
  • Maarifa ya programu za ofisi (Word, Excel, PowerPoint, Email, Publisher n.k.)
  • Mafunzo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali

Mshahara: TGS C

2. Dereva Daraja II – Nafasi 4

Majukumu ya Kazi:

  • Kukagua usalama wa gari kabla na baada ya safari
  • Kuwasafirisha watumishi kikazi
  • Kufanya matengenezo madogo ya gari
  • Kutunza log book ya safari
  • Kusambaza nyaraka na kufanya usafi wa gari
  • Majukumu mengine kutoka kwa msimamizi

Sifa za Mwombaji:

  • Elimu ya Kidato cha IV
  • Leseni ya Daraja E au C
  • Uzoefu wa mwaka 1 bila kusababisha ajali
  • Cheti cha Basic Driving Course kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa

Mshahara: TGS B

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  • Raia wa Tanzania, umri miaka 18 hadi 45
  • Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja aina ya ulemavu
  • Ambatanisha CV yenye namba za simu, email, na referees watatu
  • Ambatanisha vyeti halisi vilivyothibitishwa na wakili:
    • Cheti cha Kidato cha Nne/Sita
    • Vyeti vya taaluma na kompyuta
    • Cheti cha mafunzo ya udereva (kwa nafasi ya Dereva)
  • Testimonials, Provisional Results, Statement of Results hazitakubaliwa
  • Waliosoma nje wahakikishe vyeti vimeidhinishwa na NECTA, TCU au NACTVET
  • Wastaafu hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  • Watumishi wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba
  • Taarifa au vyeti vya kughushi vitasababisha hatua za kisheria
  • Tafauti za majina kwenye vyeti zirekebishwe kwa Deed Poll

Jinsi ya kutuma maombi

Mwisho wa Kutuma Maombi
Tarehe ya mwisho: 14/08/2025

Namna ya Kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kwa njia ya mfumo wa kielektroniki kupitia:
https://portal.ajira.go.tz

Anuani ya barua ya maombi:
Mkurugenzi wa Mji
S.L.P 383
BABATI

Maombi yasiyotumwa kwa mfumo huu hayatafanyiwa kazi.

Soma zaidi: