Hili hapa tangazo la Nafasi 21 za Ajira Mpya MDAs & LGAs. Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Wizara, Idara zinazo jitegemea, Wakala za Serikali, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi ishirini na moja (21) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
Nafasi zilizotangazwa leo
1. Mhasibu daraja la pili – Nafasi 20
- Kuandika taarifa ya mapato na matumizi;
- Kuandika taarifa za maduhuli;
- Kupokea maduhuli ya serikali na kupeleka Benki kwa wakati;
- Kufanya usuluhisho wa hesabu za Benki na nyingine zinazohusiana na masuala ya fedha;
- Kukagua hati za malipo; na
- Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
- Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Sita wenye shahada ya Uhasibu au Biashara waliojiimarisha kwenye fani ya Uhasibu au Stashahada ya juu ya Uhasibu kutoka Taasisi inayotambuliwa na Serikali pamoja na cheti cha 2 Taaaluma ya Uhasibu CPA(T) au sifa inayolingananayo inayotambuliwa na NBAA.
2. Nahodha daraja la pili – Nafasi 1
- Kubuni na kuunda zana za kuvulia samaki (Fishing Gears);
- Kutunza na kutengeneza zana za kuvulia samaki;
- Kuongoza na kuendesha meli/boti ndogo za futi 40 zenye uzito wa kuandikishwa wa tani 50-200 (GRT); na
- Kuendesha shughuli za uvuvi katika meli/boti.
- Kuajiriwa wenye Stashahada (Diploma) ya Unahodha na Uvuvi ( Master Fisherman) kutoka Chuo cha Uvuvi Mbegani au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Jinsi ya kutuma maombi
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 11 Mei, 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments